Majaji wa Kifaransa wawasili Rwanda kuhusu mauaji ya kiholela
24 Novemba 2009Matangazo
Baada ya Ujerumani kuwatia mbaroni karibuni Wa-Nyarwanda wawili wanaoshukiwa kwa mauaji ya halaiki, ubakaji na uporaji katika eneo la mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Rwanda, hivi sasa wamewasili mjini Kigali majaji wawili wa Kifaransa kufanya uchunguzi dhidi ya washukiwa wakubwa wanne, ambao wanatuhumiwa na wakuu wa Rwanda kuhusika na mauaji ya kiholela katika nchi hiyo. Majaji hao wa Kifaransa, Michele Ganascia na Fabinene Puos, hadi sasa hawajawaambia lolote waandishi wa habari. Othman Miraji punde hivi alizungumza na mwendeshaji mkuu wa mashtaka wa Rwanda, Martin Ngoga, kutaka kujua zaidi juu ya shughuli za Wafaransa hao hapo Kigali:
Mtayarishaji: Othman Miraji
Mpitiaji: Mohamed Abdulrahman