Mahojiano na Balozi Ali Karume juu ya mchakato wa kutafuta mtetezi wa CCM kwa urais wa Zanzibar | Matukio ya Kisiasa | DW | 05.07.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mahojiano na Balozi Ali Karume juu ya mchakato wa kutafuta mtetezi wa CCM kwa urais wa Zanzibar

Mwishoni mwa wiki, kamati maalum ya Chama tawala cha mapinduzi, CCM, huko Visiwani Zanzibar ilikutana kuyajadili majina ya wanachama 11 wanaotaka kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Kati ya majina hayo kuna waziri kiongozi wa zamani, Mohammed Gharib Bilal; makamo wa rais wa Jamhuri ya Muungano, Dr. Ali Sheni; waziri kiongozi wa sasa, Shamsi Nahodha; makamo wa waziri kiongozi wa sasa, Ali Juma Shamhuna, na Balozi Ali Karume, ndugu wa rais wa sasa wa Visiwani Zanzibar, Amani Karume.

Othman Miraji punde hivi amezungumza na Balozi Ali Karume na kumuuliza vipi mambo yalivokwenda katika mkakati wa kutafuta mtetezi wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM...

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com