1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahkama yahalalisha urais wa Musharraf

20 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CJVp

Mahakimu wa Mhakama Kuu nchini Pakistan waliochaguliwa binafsi na Rais Pervez Musharraf hapo jana imewachukuwa masaa mawili tu kutupilia mbali changamoto za kisheria dhidi ya kuchaguliwa kwake tena kuwa rais wa Pakistan.

Hukumu hiyo inafunguwa njia kwa Musharraf kun’gatuka kwenye wadhifa wa mkuu wa majeshi hivi karibuni na pengine kuregeza utawala wa hali ya hatari ambao umeathiri vibaya uhusiano wake na Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Benazir Bhutto na Marekani.

Hukumu hiyo pia imewakasirisha wapinzani wake wakuu ambao wanasema nchi nzima imewekwa kwenye utawala wa sheria za kijeshi kwa sababu tu ya kupata uamuzi huo na kwamba baada ya Musharraf kupata uamuzi wake huo chini ya mtutu wa bunduki huenda akawa tayari kufikia muafaka.

Musharraf ametaka uchaguzi wa bunge nchini humo ufanyike nchini humo hapo tarehe 8 mwezi wa Januari.