Mahdi azuiliwa kurejea Misri
2 Julai 2018Matangazo
Chama cha Umma kinachoongozwa na Mahdi kimesema vyombo vya usalama vilimzuwia waziri mkuu huyo wa zamani wa Sudan kuingia Misri wakati akirejea kwenye mkutano wa upinzani mjini Berlin, Ujerumani.
Mahdi, ambaye amekuwa akiishi mjini Cairo, alisafiri kwenda London na mwanawe wa kike, Mariam, pamoja na msaidizi wake.
Akihusika sana katika siasa nchini Sudan tangu miaka ya 1960, Mahdi alikuwa waziri mkuu kuanzia mwaka 1966 hadi 1967 na tena mwaka 1986 hadi 1989.
Serikali yake ilikuwa ya mwisho kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia nchini Sudan, kabla ya kuangushwa katika mapinduzi mwaka 1989 yaliyofanywa na rais wa sasa, Omar Hassan al-Bashir.