1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maharamia waiteka meli ya Algeria

3 Januari 2011

Meli ya MV Blida ilitekwa katika pwani ya Oman

https://p.dw.com/p/zt4R

Maharamia wa Kisomali wanashukiwa kuwa wameiteka nyara meli moja ya Algeria iliyokuwa na mabaharia 27 iliyokuwa kwenye bahari ya Hindi. Kulingana na kitengo cha Umoja wa Ulaya cha kupambana na uharamia, MV Blida, ilitekwa nyara Jumamosi ilipokuwa umbali wa kiasi ya maili 150 kusini mashariki mwa bandari ya Oman ya Salalah. Meli hiyo ilikuwa inaelekea Tanzania ilipotekwa nyara. Mabaharia hao wanatokea Algeria, Ukraine na Ufilipino.