1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama yathibitisha ushindi wa Azali Assoumani

Bruce Amani
3 Aprili 2019

Mahakama ya juu visiwani Komoro imemthibitisha Azali Assoumani kuwa mshindi wa matokeo ya urais ya uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita katika visiwa hivyo vinavyoshuhudia hali tete.

https://p.dw.com/p/3GAad
Wahlkampf auf den Komoren
Picha: AFP/Getty Images/S. de Sakutin

Azali alitangazwa mshindi kwa kupata asilimia 59 ya kura dhidi ya mpinzani wake Mohammoudou Ahamada aliyenyakua asilimia 15.7 ya kura na Mouigni Baraka Said Souilihi alichukua nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 5.5 ya kura.

Jaji wa mahakama ya juu Harmia Ahmed akitangaza uamuzi wa mahakama hiyo alisema kutokana na Azali Asoumani kupata wingi mkubwa wa kura anatangazwa rais wa jamhuri ya visiwa vya Comoro.

Matokeo hayo yaliidhinishwa katika mahakama kukiwa na usalama wa hali ya juu mjini Moroni.

Upinzani umelalamika kwamba kulikuweko na wizi mkubwa wa kura na dosari chungunzima katika  uchaguzi uliofanyika Machi 24.

Waangalizi na mashirika ya kijamii yamehoji uhalali wa uchaguzi huo.