SiasaHong Kong
Mahakama ya Hong Kong yampata na hatia Jimmy Lai
15 Desemba 2025
Matangazo
Hii ni kesi muhimu zaidi inayohusu sheria tata ya Usalama wa Taifa iliyowekwa na China. Jimmy Lai mwenye umri wa miaka 78, anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kuchochea maandamano ya mwaka 2019 ya kudai demokrasia ambayo yalichukuliwa kama changamoto kubwa kwa utawala wa Beijing.
Viongozi wa Ulaya, Marekani na hata mashirika ya kutetea haki za binaadamu wamekosoa hatua hiyo ya Mahakama wakisema imechochewa kisiasa, huku China ikiipongeza Hong Kong kwa kuadhibu kile ilichotaja kuwa "vitendo vya uhalifu vinavyohatarisha usalama wa taifa".