Mahakama Kenya yapinga kupima mashoga | Masuala ya Jamii | DW | 23.03.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Mahakama Kenya yapinga kupima mashoga

Shauri lilikuwa limewasilishwa katika mahakama ya rufaa na shirika la kutetea haki za mashoga na wasagaji, baada ya wanaume wawili kukamatwa wakishukiwa kujihusisha na mapenzi ya watu wa jinsia moja.

Kitendo hicho kulingana na sheria za Kenya ni uhalifu ambao adhabu yake inaweza kufikia kifungo cha miaka 14 jela. Washukiwa hao wamesema walilazimishwa kupimwa sehemu zao za kutolea haja kubwa, na kuchukuliwa vipimo vya UKIMWI katika hospitali moja kwenye mji wa mwambao wa Mombasa, na kwamba maafisa wa usalama walihusika katika zoezi hilo. Shirika za kutetea haki za mashoga na wasagaji linapinga kupimwa kwa lazima kwa mashoga, likisema vitendo hivyo vinakwenda kinyume na haki zao za faragha na heshima zao za kiutu, na kwamba zinaweza kuchuliwa kama kufanyiwa mateso.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com