Magufuli atangaza baraza ′dogo′ la mawaziri | Matukio ya Afrika | DW | 10.12.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Magufuli atangaza baraza 'dogo' la mawaziri

Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametangaza baraza lake la mawaziri likiwa na mawaziri 19 na wizara nyengine zikiwa hazina hata manaibu waziri ili kupunguza gharama.

Rais John Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais John Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akitangaza baraza hilo leo (Disemba 10) Ikulu ya Magogoni, jijini Dar es Salaam, Magufuli alisema zilikuwa zimetengwa shilingi bilioni 2 ili mawaziri watakapoteuliwa waende semina elekezi, lakini baraza lake halitakuwa na semina hiyo badala yake fedha hizo zitaelekezwa kwenye sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure.

Mwandishi: Mohammed Khelef
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com