Mageuzi makubwa kufanywa katika jeshi la Ujerumani | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 24.08.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Mageuzi makubwa kufanywa katika jeshi la Ujerumani

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Karl-Theodor zu Guttenberg amewasilisha mapendekezo ya kufanywa mageuzi katika jeshi la Ujerumani "Bundeswehr."Hayo yatakuwa mageuzi makubwa kabisa katika historia ya jeshi la Ujerumani."

Verteidigungsminister Karl-Theodor zu Guttenberg (CSU), aufgenommen am Montag, 23. August 2010, im Paul-Loebe-Haus in Berlin. (apn Photo/Berthold Stadler)

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Karl-Theodor zu Guttenberg.

Waziri Guttenberg amesema, anataka kupunguza idadi ya wanajeshi kwa theluthi moja yaani kutoka 250,000 hadi kama 163,000. Vile vile amependekeza kuondoa utaratibu wa kuandikisha wanajeshi kwa mujibu wa sheria, lakini amesema, sheria hiyo isiondoshwe bali iendelee kubakia katika katiba ya nchi. Kwa kufanya mageuzi hayo, jeshi litapunguza gharama zake na litakuwa na vikosi vilivyoandaliwa bora zaidi kwa operesheni zake na bila ya kuhatarisha usalama wa ndani alieleza waziri wa ulinzi Karl-Theodor zu Guttenberg.

Mwandishi: P.Martin/ZPR

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com