Magazetini | Magazetini | DW | 16.11.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazeti ya Ujerumani

Magazetini

Mkutano kuhusu tabia nchi unaomalizika Ijumaa,Mazungumzo ya kutafuta maafikiano kabla ya kuunda serikali ya mseto ujerumani na Zimbabwe ndio mada zilizoandikwa na wahariri wa Ujerumani

BG Mugabe, First Lady Grace chat with Chinese Ambassador to Zimbabwe Qi Shunkang, 2012 (picture-alliance/Photoshot/Li Ping)

China imewekeza mabilioni nchini Zimbabwe

Mhariri wa Mittelbayerische Zeitung,)i anaandika.. 

Kansela Angela Merkel hapo jana hakuweza kungara hata kidogo kama kansela wa Mazingira na hilo linatokana na ule ukweli kwamba watu walishatambua kwamba kiongozi huyo wa serikali ya Ujerumani hatokuwa na cha zaidi ya kutowa mapendekezo ya maazimio mazuri.Na juu ya hilo Ujerumani yenyewe bado inakishindo kikubwa cha kukahikisha inafikia malengo yake ya kimazingira.Na kuhusu hatua madhubuti za kuchukua kuhusiana na suala zima la kuyalinda mazingira hasa kama mwanzilishi juhudi zake zinakabiliwa na kishindo kikubwa mjini Berlin.

Kuhusu  Zimbabwe mhariri wa  Reutlinger General-Anzeiger  anasema -

Ziara ya Amiri mkuu wa majeshi Generali Chiwenga siku za hivi karibuni mjini Beijing -si bure-ndo kusema mapinduzi yaliyofuatia baadae hayakutokea hivihivi tu,yalikuwa yameshapata ridhaa.Hapana shaka yoyote kwamba China imewekeza mabilioni nchini Zimbabwe  kwa sababu inakiu kikubwa mno cha rasilimali ya nchi hiyo.Kipindi chote cha Mugabe kususiwa na nchi za Magharibi aliitegemea China.China pia katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa imekuwa ikiingia kifua Zimbabwe na Mugabe.Kwa hivyo mtu anaweza kuamini kwamba Mugabe ni kipenzi cha serikali ya mjini Beijing.

Badische Tagblatt linaandika

Huu pia ni msimu wa mwisho wa mapukutiko kwa rais mkongwe wa Zimbabwe.Rais Mugabe amelikoroga na kuliharibu -ameporomoka kama shujaa katika jukwaa la siasa za nchi yake na pia kama mtu aliyeangaliwa katika historia ya Zimbabwe.Mugabe aliipa matumaini makubwa nchi yake alipoingia madarakani baada ya uhuru na kuendelea kubakia madarakani kwa kutumia kila mbinu.Suali ni ikiwa je hali ya Zimabwe itabadilika na kuwa bora baada ya mapinduzi?Suali hili lakini hakuna hata mmoja mwenye kifua cha kuliuliza nchini Zimbabwe kwasababu  labda mambo yakawa mabaya zaidi.

Straubiger Tagblatt linazungumzia kuhusu mazungumzo ya kusaka mwelekeo wa kufikia lengo la kuunda serikali ya mseto nchini Ujerumani mhariri anaandika

Kwa hakika hakuna hata mmoja,hata Kansela Angela Merkel mwenyewe na chama chake cha CDU wanaotaka kuitishwe uchaguzi mpya Ujerumani.Vyama vyote vinne havitaki abadan asilan kufikia huko na kila mmoja yuko radhi kufanya kila awezalo kuepusha balaa.Kwa maana hiyo usiku wa kesho utakuwa ni kipindi cha lala salama au unaweza kusema hakutolalika mpaka kieleweke.Na hasa itabidi upatikane mwafaka kuhusu suala la wakimbizi,ulinzi wa mazingira na suala la kuungana familia.Lakini mwisho wa yote hayo mwafaka wa vyama vyote ndio unaotakiwa.Mengine yote hakuna raia yoyote Ujerumani yanayomshughulisha.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri . Mohammed Abdul-rahman

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com