1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini: Trump kushitakiwa bungeni

Sekione Kitojo
23 Agosti 2018

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha zaidi leo (23.08.2018)na mada kuhusu kitisho cha kushitakiwa Trump bungeni, na pia kuhusu msaada kwa wakulima baada ya ukame ulioikumba Ulaya  hivi karibuni.

https://p.dw.com/p/33d2Y
Kombi-Bild - USA Russland-Affäre - Donald Trump, Michael Cohen und Stormy Daniels
Picha: picture alliance/AP

Tukianza  na  gazeti  la  Die Rheinpfalz  la  mjini  Ludwigshafen, mhariri  anasema  pekee suala  la  Cohen linatosha  kumshitaki  rais Trump  katika  baraza  la  Congress. Mhariri  anaandika:

"Chama  cha  rais  Trump  cha  Republican ambacho  kina  wingi bungeni  kwa  sasa, kitataka  kufanya  mambo  ya  uadui. Wanahofia kwamba  kundi la chama  hicho la  siasa kali  za  mrengo  wa  kulia linalomuunga  mkono  kwa  dhati Trump linapaswa  kuendelea kumuunga  mkono. Katika demokrasia  inayofanya  kazi  ni  lazima uongo  wa  rais  na  ufuasi  wa  woga  kuhusu kampeni  ya  chama chake  kuwa  mada  namba  moja. Chama  cha  Democratic ni lazima kijitahidi  kupata  wingi, mwanzoni  mwa  mwaka  ujao wa 2019  na  kuanza muhula  mpya  wa  baraza  la  Congress kwa  kuwa na  wingi  wa  kutosha  ili  kuweza kumshitaki  bungeni  rais. Lakini hata  hivyo  inahitajika  kwa  mujibu  wa  katiba , baraza  la  Seneti likubali kwa  wingi  wa  theluthi mbili , ili  kuweza  kumtangaza Trump kuwa  ana makosa  na  kumuondoa  kutoka  madarakani."

Gazeti la Südwest Presse kuhusu  mada  hiyo  linaandika kwamba Cohen na  Manafort  pekee  hawawezi  kufikisha  rais  wa  Marekani katika  hali  ya  kuanguka  kutoka  madarakani. Mhariri  anaandika:

"Lakini  wamezusha  maporomoko, ambayo kwa  njia  moja  ama nyingine  yanaweza  kuwa  na  athari  kwa  Trump. Kitu  muhimu kitakuwa , iwapo  chama  cha  Democratic  mwezi  Novemba takriban  katika  baraza  moja  la  bunge  kitakuwa  na  wingi. Wanapaswa  kwa  hiyo  kufanya  kila  linalowezekana, kumfikisha rais  Donald  Trump  katika  hali  ya  kushitakiwa bungeni."

Kwa  sasa  hakuna  ushahidi wa  mazungumzo  yaliyofanyika  kati ya  kampeni ya  Trump  na  Urusi, anaandika  mhariri wa  gazeti  la Frankfurter Rundschau. Kwa  hivi  sasa  rais Trump  anashutumiwa kuhusiana na fedha  alizotoa ili  kumnyamazisha mwanamke aliyekuwa  na  mahusiano  nae kitu ambacho  ni  kinyume  na  sheria za  fedha  za  michango  kwa  ajili  ya  chama. Mhariri  anaandika:

"Katika  nchi  nyingine  hali  hiyo  ingezusha  mzozo  katika  serikali. Nchini  Marekani  wafuasi  wa  Trump  wanamshangiria shujaa  wao , na  chama  chao na  kutupilia  mbali msingi  yake. Hatua  ya kushitakiwa  bungeni  kwa  hiyo  haipo. Iwapo  kutakuwa  na mabadiliko  katika  wingi wa wabunge  bungeni  katika  uchaguzi  wa bunge  mwezi  Novemba , suala  hilo  litakuwa  na  sura  nyingine. Mambo  mengi  yatahusiana  na  kazi  anayofanya  Mueller  ambaye ndiye anahusika  na  uchunguzi  wa  suala  hilo pamoja  na  Trump binafsi." 

Mhariri  wa  gazeti  la  Stuttgarter Zeitung anazungumzia  kuhusu  hali ya  ukame  iliyolikumba  bara  la  Ulaya  katika  majira  haya  ya kiangazi. Mhariri  anazungumzia  kuhusu  uamuzi  wa  serikali kuwapa  msaada  wakulima  kutokana  na  ukame. Mhariri anaandika:

"Waziri  wa  kilimo Kloekner kwa  msaada  huu  wa  haraka  hapaswi kusita. Hali  mbaya  ya  hewa  ya  majira  ya  joto sio moja kwa  moja matokeo  ya  mabadiliko  ya  tabia  nchi, licha  ya  kwamba  idara  ya hali  ya  hewa  ya  Ujerumani  inaliangalia  suala  hili  la  joto  kali ambalo halikuwa  la  kawaida  tangu  mwaka  1881 kwa  jicho  hilo. Pamoja  na  hayo  lakini  hakuna  kitakachobadilika, kwamba  sekta ya  kilimo, kama  ilivyo  sekta  ya utoaji  wa  nishati  ama usafirishaji, zilivyojielekeza kupambana  na  mabadiliko  hayo. Na kutokana  na  hayo  kuna  nafasi  kubwa  kwa  jamii  na  pia  kwa wakulima kufaidika."

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / inlandspresse / Deutschland

Mhariri: Iddi Ssessanga