Magazetini: Kramp-Karrenbauer na hatimaya yake | Magazetini | DW | 22.07.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Magazetini: Kramp-Karrenbauer na hatimaya yake

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanazungumzia kuhusu nyadhifa alizonazo mwenyekiti ya chama cha CDU Annegret Kramp-Karrenbauer kuwa huenda zikawa kikwazo kwa mustakabali wake, mivutano katika mlango  bahari wa Hormuz. 

 Tuanze  na  gazeti  la Neue Osnabrueker Zeitung akizungumzia kuhusu wasi wasi  katika  masuala  ya  kiusalama katika uandikishaji wanajeshi  katika  jeshi  la  Ujerumani. Mhariri  anaandika:

 

"Katika  muda  wa  miaka  miwili ni  wanajeshi 21 tu ambao  walitaka kujiunga  na  jeshi  la  Ujerumani waliondolewa  kupitia  uchunguzi, kwasababu  walikuwa  ni  wenye msimamo  mkali  wa  mrengo  wa kulia. Idadi  hiyo  ndogo  ya  walioondolewa  pamoja na mmoja ambaye alituhumiwa, haiakisi kiwango  kilichopo. Tatizo  kubwa bado  ni  kuhusu  kile  wanajeshi  ambao  bado  wamo  katika  jeshi wanachokiwakilisha. Waziri wa  zamani  wa  ulinzi Von der Leyen alikosoa  tatizo  la  mitazamo  ya wanajeshi. Mrithi  wake  Annegret Kram-Karrenbauer kwa  upande wake  anazungumzia kwamba haiwezekani  kuwaweka wanajeshi  wote  kuwa  washukiwa. Kwa hilo Kramp-Karrenbauer  anajitenga  na  kosa  kubwa la  matamshi ya mtangulizi  wake."

 

Gazeti  la  Reutlinger General-Anzeiger likizungumzia  kuhusu  jeshi la  Ujerumani ameandika:

 

"Iwapo Kram-Karrnbauer  anaweza  kweli  kuokoa hali ya uaminifu wa  jeshi  la  ulinzi  la  Ujerumani, hali  hiyo inategemea  iwapo, anaweza  kutoa matamshi  sahihi  ambayo anaweza  kuyafanyia kazi. Wanajeshi watakuwa kiasi  na  shaka shaka iwapo ataweza kuweka miundo mbinu  bora  katika  jeshi. Iwapo hali  hii haitakuwapo, sauti  za  shutuma haraka  zitaanza  kuwa  kubwa , kwamba  anataka  kutumia  wizara  hiyo  ya  ulinzi  kama jiwe la kukanyaka  kurukia  katika wadhifa wa  ukansela."

US Präsident Trump in North Carolina (picture-alliance/R. Ellis)

Rais wa Marekani Donald Trump

 

Mhariri wa  gazeti  la  Frankfurter Allgemeine Zeitung anazungumzia kuhusu  suala  la  Iran kuwa  katika  mvutano  na  mataifa  ya magharibi. Mhariri  ansema  tangu  pale  rais  wa  Marekani  Donald Trump  kuiondoa nchi  yake  katika  makubaliano  ya  kinyuklia, hali ya mashariki  ya  kati sasa  inaonekana hivi : Mhariri  anaandika:

 

"Iran  ilichukua  hatua za  kimapambano  zaidi kuelekea  mataifa  ya Kiarabu, lakini mpango wake  wa  kinyuklia  ulikuwa  chini  ya  udhibiti wa  kimataifa. Leo hii  Iran inachukua  tena hatua za  kimapambano zaidi kwa  mataifa  ya  Kiarabu  na  inajenga upya mpango  wake  wa kinyuklia, na inavuruga  njia  muhimu  kwa  ajili  ya  uchumi,  njia inayopita meli  za  kibiashara  katika  mlango bahari  wa  Hormuz. Mhariri  anaandika  kwamba  hapa  ni  lazima  kupambana. Ujerumani na  Ufaransa kwa  mara  ya  kwanza  mwishoni  mwa  juma , zimejiweka  upande  wa  Uingereza. Hii ni  hatua  nzuri. Kwa wastani Iran inataka  sasa kuzigawa  nchi  za  Ulaya. Pamoja  na  hayo ni lazima  tukubali  kuwa  funguo  wa  matatizo  haya  yote uko mikononi mwa  Marekani."