Magazetini: Hukumu dhidi ya kundi la Freital ,hapa Ujerumani | Magazetini | DW | 08.03.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Magazetini: Hukumu dhidi ya kundi la Freital ,hapa Ujerumani

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha zaidi na hukumu iliyotolewa dhidi ya kundi la siasa kali za mrengo wa kulia mjini Freital, kitisho cha vita vya kibiashara kati ya Marekani na mataifa mengine duniani.

Dresden - Urteile im Prozess gegen «Gruppe Freital» (picture-alliance/dpa/S. Kahnert)

Mahakamani wakati wa kutoa hukumu dhidi ya kundi linalojulikana kama Freital la wanazi mamboleo

Gazeti  la  Badische Zeitung la  mjini  Freiburg kuhusiana  na  hukumu  iliyotolewa  dhidi  ya  kundi  linalojulikana kama Freital  la msimamo mikali ya  mrengo  wa  kulia, gazeti linaandika.

Kutokana  na  hukumu dhidi ya  wanachama  wa  kundi  ambalo sio tu walikuwa  wakijaribu kuuwa, na  hata  kujenga  kundi la kigaidi, hatua zimechukuliwa na  msingi wa  kuzima  hali  hiyo umewekwa.  Hata  wale  ambao  wameacha  ugaidi ni magaidi. Mashitaka  yaliwahusu  kundi  lililojificha  katika ulinzi eti wa  umma na  baadaye  kuzungumza  katika  mitandao  ya  kijamii  kama makundi  kwa  siri  wakitaka  kufanya  mashambulizi ya  miripuko, hawawezi  kusingizia, kwamba  walikuwa  tu ni  baadhi ya  watu waliokubaliana  kufanya  hivyo na  sio  wote waliotaka  kuwauwa watu  waliokuwa  wakiomba  hifadhi.  Ndio, ni kweli :  kumekuwa  hivi karibuni  katika  maeneo  ya  Ujerumani  mashariki  na  maandamano makubwa. Ambapo waungwaji  wake  mkono  walikuwa wakitoa  kauli mbiu iliyokuwa  inakera , lakini  kutokana  na  uhuru wa  kutoa  maoni  haikuweza  kuzimwa. Hawakuonekana  kuwa  wanakwenda kinyume  na ubinadamu.

Kila  mmoja  katika  Freital alifahamu  kuhusiana  na uhalifu  wa kundi  la  wanazi mamboleo, ni  polisi  tu hawakuwa  na  habari. Anaandika  mhariri  wa  gazeti  la  Märkische Oderzeitung  la  mjini Frankfurt / Oder akizungumzia  kuhusu  hukumu  hiyo  iliyotolewa dhidi  ya  kundi  la  kigaidi  ya  wanazi mamboleo mjini  Freital. Mhariri  anaandika.

Dresden - Urteile im Prozess gegen «Gruppe Freital» (picture-alliance/dpa/S. Kahnert)

Mmoja kati ya walifu wa kundi la Freital akifikishwa mahakamani

Kuna maafisa  wengi  wanaowaunga  mkono  magaidi. Takriban polisi  mmoja  aliwahi  kuwa  mtu  anayetoa  taarifa  kwa  kundi  hilo la  misimamo  mikali  ya  mrengo  wa  kulia.  Na mahakama  ya Saxon  haikuona  hamasa  za  kisiasa  kwa  wahalifu  hao. Licha  ya mwelekeo  wa  kupinga  wakimbizi  na  makundi  ya  mrengo  wa kushoto. Lengo  gani  basi  lilitakiwa  kuonekana  hapa?  Anauliza mhariri.

Vita vya kibiashara

Kuhusiana  na  vita  vya  kibiashara  kati  ya  Umoja  wa  Ulaya  na Marekani , mhariri  wa  gazeti  la  Neue Osnabrücker  anaandika:

Halmashauri  ya  Umoja  wa  Ulaya imechukua  hatua, lakini  sio kwa hatua  ilizochukua  Marekani kwa  kutangaza  kupandisha  kodi  kwa biadhaa kama  chuma  cha  pua na  aluminium. Ni sawa kwani cheche  huzaa  moto. Hiki  ni  kitisho  cha  vita  ya  kibiashara, ambayo  ni  mshindwa  tu anafahamu.  Kuonesha  ishara  ni  muhimu. Ni  kwa  njia  hiyo  tu huenda  rais  wa  Marekani Donald Trump , anaweza  kutambua, ni wapi kujihami kimasoko  kunaweza kumpeleka. Lakini  iwapo Umoja  wa  ulaya  inaongeza  kodi  kwa biadhaa  kama  siagi ya karanga, vinjwaji vikali kama  wiski, nguo za Jeans na pikipiki, kwa  mtazamo wa  haraka  inaonekana  kama ni hatua  dhaifu. Hizi hata  hivyo  ni bidhaa  maarufu  sana  za Marekani. Na hatua  hizi zinaleta  hali  ya  tahadhari.

Iwapo inawezekana  kumzuwia  rais Trump  kwa  kupandisha  kodi za  bidhaa  kama  juisi  ya  machungwa  kutoka  Califonia ama Cranberi, itabidi  kusubiri  na  kuona.  Anaandika  mhariri  wa  gazeti la  Rhein-Zeitung  la  mjini  Koblenz kuhusiana  na  kitisho cha  vita ya  kibiashara kati  ya  Marekani  na  Umoja  wa  Ulaya. Mhariri anaandika.

Hatari  inaonekana  zaidi  katika  kuweka ongezeko  la  kodi  katika kila  bidhaa. Kwa  hatua  kama  hizo  hakuna  atakayeshinda.  Trump hawezi kupata faida kwa upande  wa  biashara  ya  chuma cha  pua na  Umoja  wa  Ulaya  hautaweza  kufikia  katika  lengo  la  soko huru.

Ukiukaji  mkubwa  wa  haki  za  binadamu  hauvifikii  vyombo  vingi vya  habari. Anaandika  mhariri  wa  gazeti  la  Weser-Kurier  la  mjini Bremen  kuhusiana  na  ripoti  ya  haki  za  binadamu  ya  Umoja wa mataifa. Mhariri  anaandika:

Hakua  taarifa  zilizojitokeza  za  uhuru  wa  kutoa  habari  nchini Cambodia  muda  mfupi  kabla  ya  uchaguzi. Hakuna  mtu  aliyejua, kwamba  wanawake  nchini  El Salvador  wanahukumiwa  kifungo cha  muda  mrefu, inapotokea  ujauzito umetoka. Masuala  ya kisiasa  pia  yanaundumila  kuwili. Umoja  wa  Ulaya  umeweka vikwazo vya  kisiasa  kwa  utawala  wa  Venezuela, lakini  watu wengi  hawawezi  kutoa  kauli  zao  nchini  Ukraine. Mhariri  anasema suala  la  haki  za  binadamu  limechukua  mtazamo  wa  kimaslahi zaidi.

 

Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com