Magaidi wawaua maafisa usalama Mogadishu | Matukio ya Afrika | DW | 05.03.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Magaidi wawaua maafisa usalama Mogadishu

Magaidi wa kundi la itikadi kali la Al-Shabaab wamewaua maafisa wasiopungua wanane na kuwajeruhi wengine kadhaa baada ya kulivamia gereza na kusababisha wafungwa kadhaa kutoroka.

Maafisa wa usalama wasiopungua 8 wameuwawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya kundi la itikadi kali la Al-Shaabab kufanya uvamizi kwenye jela moja kaskazini mwa Somalia usiku wa kuamkia leo.

Afisa wa polisi aliyetambulishwa kwa jina la Hussein Ali ameliambia shirika la habari la DPA kuwa wakati wa uvamizi huo  wafungwa kadhaa ikiwemo watu wanaoshukiwa kwa ugaidi wametoroka.

Kulingana na Hussein shambulizi hilo lilianza kwa mripuko mkubwa na kisha wanamgambo wenye silaha nzito walivamia gereza la mji wa bandari wa Bosaso kwenye jimbo la Puntland usiku wa manane.

Kundi la Al-Shabaab limethibitisha kuhusika na uvamizi huo kupitia matamshi liliyoyatoa kwenye kituo cha redio kinachounga mkono harakati zake likisema limewasaidia wafungwa 400 kutoroka.