Mafuriko Pakistan , watu zaidi ya 800 wafariki | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 01.08.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mafuriko Pakistan , watu zaidi ya 800 wafariki

Zaidi ya watu 800 wamepoteza maisha yao katika mafuriko mabaya kuwahi kutokea kaskazini magharibi ya Pakistan

default

Wanakijiji nchini Pakistani wakihangaika kutaka kufika katika maeneo ya salama kutokana na mafuriko mabaya kabisa kuwahi kutokea nchini humo.

Zaidi ya watu 800 wamepoteza maisha yao katika mafuriko mabaya kabisa kutokea kaskazini-magharibi ya Pakistan katika kipindi cha miaka 80 iliyopita. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa takriban watu milioni moja wameathirika kwa mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa za msimu wa masika.

Waokozi kutoka Pakistan na nchi jirani ya Afghanistan wanawatafuta wakaazi waliokwama  katika vijiji vilivyozingirwa na maji. Ripoti zinasema watu 60 wameuawa katika eneo hilo. Madaraja yaliyobomoka na barabara zilizofurika zinachalewesha kazi za wasaidizi wanaotaka kupeleka misaada kwa wahanga waliokwama vijijini.

Umoja wa Mataifa umeahidi kupeleka misaada ya kiutu kwa wale walioathirika. Serikali ya Ujerumani imezidisha msaada wake kufikia Euro milioni 1. Wakati huo huo Umoja wa Ulaya utatoa msaada wa Euro milioni 30.Kwa mujibu wa idara ya utabiri  wa hali ya hewa, mvua huenda zikaendelea kunyesha kwa hadi siku kumi zingine.

 • Tarehe 01.08.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OZEC
 • Tarehe 01.08.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OZEC
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com