1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Maelfu wakusanyika Sao Paulo kumuunga mkono Bolsonaro

26 Februari 2024

Maelfu ya watu wamekusanyika katika barabara maarufu ya Paulista mjini Sao Paulo kama ishara ya kumuunga mkono rais wa zamani Jair Bolsonaro.

https://p.dw.com/p/4csE2
Brazil | Sao Paulo | Jair Bolsonaro | Wafuasi wa Jair Bolsonaro
Wafuasi wa Rais wa zamani wa Brazil Jair BolsonaroPicha: Andre Penner/AP Photo/picture alliance

Mkusanyiko huo unatokea katika wakati uchunguzi unaendelea kuhusu madai kwamba kiongozi huyo alipanga njama ya mapinduzi ili kusalia madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 2022.

Bolsonaro anayeegema siasa za mrengo wa kulia, aliitisha mkutano huo baada ya kulengwa na msako wa polisi mapema mwaka huu.

Kiongozi huyo alihutubia kwa takriban dakika 20 na kukanusha madai dhidi yake.

Polisi inamtuhumu kwa kuongoza njama iliyofeli ya kutaka kusalia madarakani baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu uliopita na mpinzani wake Rais Luiz Inacio Lula da Silva.

Jair Bolsonaro ameeleza kuwa, tuhuma hizo zimechochewa kisiasa.