1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu ya wakimbizi watoroka vita Kongo

24 Juni 2022

Idadi ya wakimbizi wanaokimbia mapigano yanayoendelea kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Kongo na kundi la waasi wa M23 katika wilaya ya Rutshuru kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini imepindukia watu elfu 30.

https://p.dw.com/p/4DChs
DR Kongo Flüchtlinge
Picha: AFP via Getty Images

Wanaokimbilia ndani ya vijiji vinavyodhaniwa kuwa na usalama ikiwemo kijiji cha Rumwangabo mbali kidogo na makao makuu ya wilaya hiyo ambamo mamia wengine wanahangaishwa na ukosefu wa chakula pamoja na maji safi.

soma Amnesty: Raia lazima walindwe Kongo

Mapigano ya hivi karibuni katika vijiji vya Ruvumu ,Chengerero na ambayo yaliendelea hadi jana jioni katika eneo la Nkokwe yamesababisha maelfu ya watu kutoroka makwao ili kutafuta hifadhi katika maeneo tofauti ikiwemo mji wa Goma pamoja na kijiji cha Rumangabo mbali kidogo na makao makuu ya wilaya hiyo ambamo mamia ya wakimbizi hao, baadhi ikiwa ni watoto na wanawake waendelea kuhangaika.

soma Wakuu wa Afrika Mashariki wakubali kupeleka jeshi, DRC

Hali inazidi kuwa mbaya

DR Kongo Flüchtlinge
Picha: ESDRAS TSONGO/AFP via Getty Images

Hadi sasa, wakimbizi hao wakiwa wameanza kupoteza matumaini ya upatikanaji wa amani  kufuatia kasi ya mashambulizi ya kundi la M23 kuendelea kuviteka baadhi ya vijiji wilayani Rutshuru hapa wanasema.

"watoto wetu wana taabika na magonjwa kila  wakati, wamekosa hata  dawa  kwa hiyo tungehitaji mashirika yakiutu yatulee misaada hata amani na usalama ili turudiye nyumbani." alisema mkimbizi mmoja

soma Wakongo na mashirika ya kiraia waliunga mkono jeshi

"hatuna maji wala dawa , hatujamuona yoyote ule anaye wasili hapa kwakutushughulikia nakututolea msaada. " mkimbizi mwengine aliiambia DW.

Katika ripoti iliyochapishwa na mashirika ya haki za binadamu mwanzoni mwa juma hili, imekadiria kuwa watu zaidi ya laki moja wametawanyika kote katika wilaya ya Rutshuru huku elfu 30 kati yao wakiwa wamepiga kambi ndani ya kijiji hiki cha Rumangabo ambamo wasiwasi umeanza pia kutanda baada ya ongezeko hilo la wakimbizi.

Mbali na hayo, watu zaidi ya 20 wameuawa kwa risasi na wengine kukatwa kwa mapanga katika kipindi cha siku tatu ndani ya kijiji cha Ruvumu eneo la Jomba, vifo ambavyo vimeshukiwa kuendeshwa na wapiganaji wa kundi la M23 ambao wamekanusha madai hayo yaliyotolewa kwenye ripoti iliyochapishwa tangu siku ya Jumatano na muungano wa asasi za kiraia wilayani Rutshuru.

 

Benjamin Kasembe