1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUkraine

Maelfu waondolewa baada ya bwawa kubwa kushambuliwa Ukraine

7 Juni 2023

Ukraine imeendelea kuwahamisha maelfu ya watu leo baada ya shambulizi dhidi ya bwawa kubwa la maji kusababisha mafuriko ya kutisha yaliyosambaratisha vijiji kadhaa na kuzusha wasiwasi wa kutokea janga la kibinadamu.

https://p.dw.com/p/4SI6i
Ukraine | Evakuierung | Nova-Kakhovka-Staudamm | Cherson
Waokoaji wakijaribu kuvuta boti iliyokuwa imewabeba wakaazi waliohamishwa kutoka Kherson, kulikoshuhudiwa mafuriko.Picha: AP/Libkos

Hadi sasa mamlaka za Ukraine zimesema zaidi ya watu 17,000 wamehamishwa na jumla ya vijiji 24 vimefurika maji tangu bwawa kubwa la Kakhovka liliposhambuliwa jana asubuhi.

Mamia ya watu bado wamekwama juu ya mapaa ya nyumba au kwenye matawi ya miti wakisubiri kuokolewa.

Urusi na Ukraine zimelaumiana kuhusika na hujuma hiyo dhidi ya bwawa hilo ambalo lilikuwa chanzo cha maji ya kupooza mitambo ya kinu kikubwa cha nyuklia barani Ulaya cha Zaporizhzhia.

Mataifa ya magharibi yameunga mkono madai ya Ukraine kwamba Urusi ndiyo imelishambulia bwawa hilo madai ambayo Moscow imesema hayana ukweli.