Maelfu wakimbia vita Jamhuri ya Afrika ya Kati | Matukio ya Afrika | DW | 07.12.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Maelfu wakimbia vita Jamhuri ya Afrika ya Kati

Zaidi ya watu 10,000 wamekimbia mapigano Jamhuri ya Afrika ya Kati. Umoja wa Mataifa unakadiria zaidi ya watu milioni moja wameyama makazi yao nchini humo na wengine milioni 2.4 wanahitaji msaada wa dharura wa chakula

Zaidi ya watu 10,000 wamekimbia mapigano Jamhuri ya Afrika ya Kati, hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu. 

Msemaji wa shirika hilo Sylivie Pellet amesema hatua hiyo inafuatia mapigano yaliyoibuka mwezi uliopita yakihusisha makundi kadhaa yaliyo na silaha karibu na mpaka wa nchi hiyo na Chad. 

Pellet amesema maelfu ya watu wanaripotiwa kuuawa katika eneo la mpaka kaskazini mwa nchi hiyo. Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Novemba lilikubali kurefusha muda wa wanajeshi wa kulinda amani nchini humo kwa mwaka mmoja zaidi na kuahidi kuongeza wanajeshi 900 ili kuzuia machafuko nchini humo. 

Umoja wa Mataifa unakadiria zaidi ya watu milioni moja wameyama makazi yao nchini humo na wengine milioni 2.4 wanahitaji msaada wa dharura wa chakula.