1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu waandamana Berlin

Kabogo Grace Patricia19 Septemba 2010

Maandamano hayo yamefanyika ikiwa ni katika kupinga hatua ya kurefushwa muda wa kutumika vinu vya nishati ya nyuklia nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/PFsk
Waandamanaji wakiwa katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin.Picha: AP

Wananchi wa Ujerumani wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo, Berlin wakipinga uamuzi wa kurefushwa muda wa kutumika vinu vya nishati ya nyuklia.

Walioandaa maandamano hayo wanasema watu 100,000 walishiriki katika maandamano hayo. Polisi wamesema kuwa watu hao walikuwa wanakaribia kufikia 40,000.

Waandamanaji hao waliandamana kupitia katika eneo la ofisi za serikali wakiizunguka ofisi ya Kansela Angela Merkel pamoja na bunge.

Utafiti unaonyesha mara kwa mara kuwa Wajerumani wengi wanapinga mpango huo wa kurefusha muda. Kansela Merkel analazimika kuhakikisha mpango huo unapita bungeni.