1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MADRID: Maelfu waandamana Uhispaniakupinga mashauriano kati ya serikali na ETA.

4 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVC

Maelfu ya watu wameandamana mjini Madrid, Uhispania, kupinga mashauriano kati ya serikali na kundi la ETA, linalowania jimbo la Basque kujitenga.

Maandamano hayo yameandaliwa na chama kikuu cha upinzani, Popular Party.

Waandamanaji wamemtaka Waziri Mkuu Jose Luis Rodriguez Zapatero wa chama cha Kisosholisti kujiuzulu kutokana na jitihada zake za kushauriana na ETA kwa nia ya kukomesha mashambulio ya kigaidi ya kundi hilo.

Kundi hilo la ETA lilivuruga mwafaka wa amani majuma matano yaliyopita kwa shambulio la bomu kwenye maegesho ya magari katika uwanja wa ndege wa Madrid.

Watu wawili raia wa Ecuador waliuawa kwenye shambulio hilo.

Waziri Mkuu Zapatero alisitisha mashauriano kati ya serikali na ETA baada ya shambulio hilo la bomu.