Madhila ya mauaji ya walemavu wa ngozi | Masuala ya Jamii | DW | 06.03.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Madhila ya mauaji ya walemavu wa ngozi

Wazazi nchini Tanzania wenye watoto walemavu wa ngozi wako mbioni kuwatafutia hifadhi baada ya utekaji na pengine mauaji ya watoto 2 kuibua hofu ya kutokea mauaji zaidi huku uchaguzi mkuu ukitarajiwa baadaye mwaka huu.

Watoto wawili wenye ulemavu wa ngozi wametoweka katika miezi miwili iliyopita licha ya serikali kuwapiga marufuku wapiga ramli wanaoshutumiwa kwa kuchochea mashambilizi ya walemavu wa ngozi kupata sehemu za miili yao zinazotumiwa kutengeneza hirizi na dawa zinazoaminiwa kuwa na nguvu za kuleta bahati nzuri na utajiri.

Februari mwaka huu polisi walipata maiti ya kijana Yohana Bahati aliyekuwa na umri wa mwaka mmoja, siku chache baada ya genge lililokuwa limejihami na silaha kumteka nyara kutoka nyumbani kwao katika eneo la Geita, kaskazini magharibi ya Tanzania. Mikono yake na miguu yake ilikuwa imenyofolewa.

Yohana Bahati alikuwa mtoto wa pili kutekwa katika kipindi cha miezi miwili katika kanda ya ziwa nchini Tanzania, ambako inakadiriwa watu 75 wenye ulemavu wa ngozi wameuwawa tangu mwaka 2000, kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa. Msichana wa umri wa miaka minne alitekwa nyara mwezi Desemba mwaka uliopita na mpaka sasa hajulikani aliko.

Katika kipindi chetu cha Maoni mbele ya meza ya duara kinachoongozwa na mwenyekiti Josephat Charo, tunazungumzia kadhia ya mauaji ya walemavu wa ngozi nchini Tanzania, changamoto na mashaka yanayowakabili watu hawa hata katika nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Kusikiliza maoni bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com