Macron na Le Pen kupambana duru ya pili | Matukio ya Kisiasa | DW | 24.04.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Ufaransa

Macron na Le Pen kupambana duru ya pili

Mgombea wa siasa za mrengo wa kati Emmanuel Macron na mgombea wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia Marine Le Pen wameingia katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa

Kwa mujibu wa matokeo ya kura, Macron amepata asilimia 23.9 ya kura na Le Pen amepata asilimia 21.4.  Kura za maoni zilizochapishwa hapo jana zinaonyesha kwamba Macron atamshinda Le Pen kwa urahisi katika duru ya pili. Akihutubia baada ya ushindi wake hapo jana Macron alisema.  Macron alisema tangu kuundwa kwa Jumuiya yake ya kisiasa mwaka mmoja uliopita, siasa za Ufaransa zimebadilika.  Kiongozi huyo amesema anataka kuwa rais atakae wawezesha watu wanaotaka kuwa wabunifu na wenye ari ya kutenda kazi ili kuyafikia malengo yao kwa urahisi na haraka zaidi.  Mgombea mwingine aliyefanikiwa kuingia katika raundi ya pili ya uchaguzi kiongozi wa chama cha mrengo mkali wa kulia Marine Le Pen amewataka Wafaransa waitumie fursa ya kihistoria iliyopo.

Präsidentschaftskandidat Marine Le Pen (picture alliance/AP Photo/F. Augstein)

Mgombea urais wa chama cha mrengo mkali wa kulia Marine Le Pen

  Le Pen amesema wakati umefika wa kuwakomboa Wafaransa kuondokana na kiburi cha tabaka la watawala. Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliochapishwa na mashirika ya IPSOS na HARRIS baada ya matokeo ya duru ya kwanza iliyofanyika jana Jumapili, asilimia kati ya 62 na 64 ya wapiga kura watapendelea Macron ashinde katika duru ya pili.

Mgombea wa chama cha kisoshalisti Benoit Hamon, Waziri mkuu wa Ufaransa Bernard Cazeneuve na mgombea urais wa chama cha kihafidhina Francois Fillon walioshindwa, wametoa mwito kwa wapiga kura wa kumuunga mkono Macron katika uchaguzi wa duru ya pili.

Juu ya ushindi wa Emmanuel Macron katika duru hiyo ya kwanza ya uchaguzi waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Sigmar Gabriel  ambaye yuko ziarani nchini Jordan amempongeza Emmanuel Macrfon kwa ushindi wake. Bwana gabriel amesema anamini kuwa inapasa kusema uchaguzi huo unatoa fursa kubwa barani Ulaya. Emmanuel Macron atakuwa rais wa Ufaransa atakae wakilisha mwanzo mpya barani Ulaya, ambaye hataridhika na hali ya mkwamo ambayo wakati mwingine huoenekana barai humu.  Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani ameongeza kusema Macron pia atazileta Ujerumani na Ufaransa ili zikaribiane zaidi.

Ufaransa sasa inakabiliwa na mvutano kati ya pande mbili baina ya Macron anayetetea sera ya kuwepo kwa Umoja wa Ulaya na katika upande mwingine Marine Le pen anayepinga uhamiaji na ambaye ameahidi kufanyika kura ya maoni juu ya Ufaransa kuendelea kuwamo au kujiondoa Umoja wa Ulaya. Le Pen amesema sasa utafanyika mjadala mkubwa na raia wa Ufaransa wataamua kati ya sera ya dunia utandawazi inayotekelezwa kwa kasi na Ufaransa yenye mipaka imara. Duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa itafanyika tarehe 7 mwezi ujao ambapo Wafaransa watamchagua kiongozi wao mpya.

Mwandishi; Zainab Aziz/DPAE/RTRE

Mhariri:Caro Robi

 

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com