Macho yote kwa Salah, Misri na Ugiriki | Michezo | DW | 26.03.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Macho yote kwa Salah, Misri na Ugiriki

Jumapili nchi kadhaa za Afrika zilikuwa na mechi za kirafiki ambapo Cameroon walikuwa wanacheza na Kuwait na mabingwa hao wa Afrika wakaebuka kidedea tatu moja.

Vincent Aboubakar na Christian Bassogog ndio waliowafungia the indomitable lions mabao yao halafu Kuwait wakafungiwa na Yaqoub Al Tararwa. Gabon nao walipata ushindi wa moja bila walipocheza na timu ya taifa ya Milki za Kiarabu.

Jumanne timu za Afrika Mashariki zitakuwa uwanjani Tanzania wakivaana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kisha Harambee stars wa Kenya wacheze na Jamhuri ya Afrika ya Kati kisha Uganda wapambane na Malawi.

Kwenye mechi zengine Afrika Misri watacheza na Ugiriki, Ivory Coast na Moldova watafute mshindi baina yao halafu Nigeria watakuwa na kazi ngumu dhidi ya Serbia. Senegal watapimana nguvu na Bosinia Herzegovina kisha Tunisia waonyeshane ubabe na Coast Rica.

Mwandishi: Jacob Safari/DPAE/Reuters/AFPE

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com