Machafuko nchini Nigeria, 300 wameshakufa. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 30.07.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Machafuko nchini Nigeria, 300 wameshakufa.

Watu 300 wameshakufa kutokana na mapigano nchini Nigeria.

default

Rais Umaru Yar'Adua amesema majeshi ya serikali sasa yanadhibiti usalama nchini Nigeria.

MAIDUGURI.

Polisi nchini Nigeria imesema watu zaidi ya 300 wameshauawa kutokana na mapambano ya siku nne baina ya majeshi ya serikali na wapiganaji wa kundi la kiislamu, kaskazini mwa Nigeria.Maalfu ya watu wamelazimika kukimbia makwao kutokana na mapigano hayo.

Maafisa wa serikali wamesema mapigano hayo yapo hasa katika mji wa Maiduguri, ambao ni makao ya kundi hilo linaloiga mfano wa taliban. Kundi hilo linapigania kutumiwa kwa sheria za kiislamu nchini Nigeria kote.

Rais Umaru Yar'Adua ameliagiza jeshi kuwazima waislamu hao mara moja.


 • Tarehe 30.07.2009
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/IzuI
 • Tarehe 30.07.2009
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/IzuI

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com