Machafuko Kyrgystan:kisa nini? | Magazetini | DW | 08.04.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Machafuko Kyrgystan:kisa nini?

Mbona wanajeshi wa Ujerumani wafariki Afghanistan? Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo , yamechambua mada mbali mbali tangu za ndani hata nje ya nchi.

default

Hamid Karzai

Kuanzia machafuko huko Kyrgystan, kutia saini leo kwa mkataba wa kupunguza silaha za nuklia kati ya rais Obama na rais Medvedev, hadi matamshi makali ya kuikosoa kambi ya magharibi aliotoa rais Hamid Karzai wa Afghanistan hivi majuzi.

Hizi ni nchi tatu za Asia ya kati zilizo masikini kabisa:Kyrgystan,Usbekistan na Tajikistan. Jamhuri hizi dhaifu kiuchumi, hazikuutumia uhuru wao kama matunda ya kujikomboa kutoka kusambaratika kwa iSoviet Union (Urusi ya zamani) kwa kujiendeleza.Ingawa uchumi unaodhibitiwa na koo mbali mbali huko umetoa sura ya demokrasia,kivitendo lakini, kila mara kukichomoza uasi na machafuko dhidi ya tawala za kimabavu .Hali ilikuwa hivyo, Usbekistan na sasa pia ni hivyo Kirgistan.Fukara zaidi tena katika kila upande, ni nchi iliopo kusini mwa nchi hizo -Afghanistan. Gazeti laendelea:

Katika eneo hilo jirani, kuna hatari inayobainisha kutokana na ugomvi wa ndani ,cheche zikawasha moto eneo zima.Itikadi kali za kiislamu zaweza zikazagaa hadi Jamhuri za zamani za kisoviet ambazo kambi ya magharibi zimeweka kambi zao kwa vita nchini Afghanistan.Je, kuna matumaini hali hii kutengenea,jibu: la hasha.

Kuhusu matamshi ya rais wake Hamid Karzai, gazeti la Mittlebayerische Zeitung linaandika kwamba, mtu asimfikirie vibaya Karzai kumuona anajaribu kujiepusha asifikwe na hatima ile ile iliomfika mtangulizi wake Mohammed Nadjibullah.Kwani gazeti laandika:

"Rais huyo wa zamani wa Afghanistan,baada ya kufunga virago na kuondoka kwa majeshi ya Urusi, aliuliwa na watalibani.Karzai kwahivyo, anaelewa enzi ya kuwapo kwa majeshi ya nchi za magharibi kumlinda nchini, ina kikomo chake. Anajua pia kuwa, bila bila ya kuungwa mkono na wakuu wa kikabila nchini hana lake katika Afghanistan baada ya kumalizika vita. Kwa hivyo, anajipanga sasa upande wao.Unaweza kumkosoa kwa ubinafsi huo.Lakini pia yafaa mtu kuhoji ila kali kutoka kambi ya magharibi upande wake."

Kuhusu mchango wa wanajeshi wa Ujerumani, katika vita vya Afghanistan, gazeti la Nordbayerischer Kurier laandika:

Kiapo "hatutaki tena vita", ni kiapo maarufu Ujerumani. Lakini, hivi sasa mbona wanakufa wanajeshi wengi wa Ujerumani, huko Afghanistan na waziri kijana wa ulinzi wa Ujerumani, anajikuta amejitwika mzigo mzito ?

Karl-Theodor zu Guttenberg, anajikuta mbele ya majeneza ya wanajeshi wa Ujerumani, waliouwawa Ijumaa ya pasaka iliopita na wajerumani wengi wanataka kukomeshwa kushiriki kwa majeshi ya Ujerumani huko Hindukusch. Vipi tutajikomboa kutoka balaa hili?

Guttenberg, alijua amechukua dhamana gani hata ikiwa sasa amepoteza imani alikuwa nayo kabla. Ametumbikia kwenye shimo kubwa ambalo hakuna ajuwae atatoka vipi.

Mwandishi: Ramadhan Ali/DPA

Uhariri: Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com