1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Machafuko Cote d'Ivoire

17 Desemba 2010

Watu 20 wanaaminika kuuawa jana baada ya makabiliano kati ya polisi waaminifu kwa Gbgabo na wafuasi wa Ouattara.

https://p.dw.com/p/Qe0Z
watu 20 wauawa katika machafuko Cote d'IvoirePicha: AP

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshtumu vikali ghasia zilizotokea nchini Cote d'Ivoire hapo jana kuhusiana na utata wa matoeko ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi jana. Kiasi ya watu 10 wanaripotiwa kuuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa wakati wa maandamano katika mji mkuu Abidjan pale wanajeshi waaminifu wa rais aliye madarakani Laurent Gbagbo walipokabiliana na wafuasi wa mpinzani wake Alassane Ouattara. Gbagbo ameng'ang'ania madaraka baada ya kushindwa na Ouattara. Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa alisema baraza hilo la usalama linaunga mkono juhudi za Umoja wa Afrika na Jumuiya ya kiuchumi katika mataifa ya Magharibi ECOWAS kujaribu kuleta utulivu Cote d'Ivoire. Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini humo wamekuwa wakijaribu kutuliza hali baada ya kuzuka kwa machafuko hayo.