1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabinti wa Lyon washinda ubingwa wa tano wa Ulaya mfululizo

Bruce Amani
31 Agosti 2020

Lyon imeshinda Kombe la Wanawake la Ligi ya Mabingwa kwa rekodi ya mara ya saba na kwa mwaka wa tano mfululizo baada ya ushindi wa  3 - 1 dhidi ya Wolfsburg jana usiku, wakati wakati ikiendelea kutawala soka la Ulaya.

https://p.dw.com/p/3hmlJ
Frauen UEFA Champions League | Finale - VfL Wolfsburg vs Olympique Lyonnais | Torjubel (0:2)
Picha: Reuters/G. Bouys

Lyon imeshinda Kombe la Wanawake la Ligi ya Mabingwa kwa rekodi ya mara ya saba na kwa mwaka wa tano mfululizo baada ya ushindi wa  3 - 1 dhidi ya Wolfsburg jana usiku, wakati wakati ikiendelea kutawala soka la Ulaya.

Klabu hiyo ya Ufaransa ilitamba katika kipindi cha kwanza kwa kufunga mabao mawili kupitia Eugenie Le Sommer na Saki Kumagai, kabla ya kuweka ulinzi mkali kuyazuia mashambulizi ya Wolfsburg wasiupeleke mchezo katika muda wa nyongeza.

Alex Popp aliifungia klabu hiyo ya Ujerumani lakini wakashindwa kuivunja ngome ya Lyon kwa mara ya pili. Sara Bjork Gunnarsdottir akaifungia Lyon katika dakika za mwisho na kuwahakikishia uhindi mjini San Sebastian. Lyon waliwafunga Wolfsburg katika fainali za 2016 na 2018, na pia kuwaondoa katika mwaka wa 2017 na 2019.