1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano yachacha Iran

Thelma Mwadzaya18 Juni 2009

Wafuasi wa mgombea wa urais wa Iran aliyeshindwa Mir Hossein Moussavi wanajiandaa kuandamana tena hii leo baada ya mwanasiasa huyo kutoa wito wa kuwakukumbuka waandamanaji waliouawa mapema wiki hii.

https://p.dw.com/p/ISSv
Maelfu wamekuwa wakiandamana mfululizo TehranPicha: AP

Vyombo vya habari vya serikali vilitangaza kuwa watu saba waliuawa wakati wa maandamano ya Jumatatu ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika wiki iliyopita.Moussavi na wafuasi wake wanashikilia kuwa matokeo hayo ya uchaguzi yana dosari.


Rais Mahmoud Ahmedinejad ametangazwa mshindi rasmi wa uchaguzi huo.Maandamano yamekuwa yakiendelea kwa siku tano mfululizo.Uongozi wa Iran kwa upande wake unasisitiza kuwa matokeo ya uchaguzi ni sahihi na kwamba serikali za mataifa ya magharibi zinaingilia mambo ya ndani ya nchi yao.


Demonstration in Berlin gegen Wahlfälschung im Iran
Wafuasi wa Moussavi wakiandamana Berlin,UjerumaniPicha: DW

Wakati huohuo Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imetangaza kuwa huenda uchaguzi wa rais wa Iran umegubikwa na utata.Kauli hiyo imetolewa na msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani Ulrich Wilhelm.Wabunge wa Ujerumani walilijadili suala hilo na hali nzima ya Iran na wanawaunga mkono waandamanaji wanaoyapinga matokeo.Kwa sasa wito umetolewa kwa uongozi wa Iran kuwaachia huru waandamanaji wanaozuiliwa,uchunguzi wa vifo vilivyotokea kufanywa pamoja na kuwaruhusu waandishi wa habari kuutangaza mvutano wenyewe uliopo.