Maandamano ya Iran | Magazetini | DW | 22.06.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maandamano ya Iran

Eti utawala wa mamullah utang'olewa kwa kishindo cha njiani?

Maandamano yakijani yamwaga damu

Maandamano yakijani yamwaga damu

Hali nchini Iran na pirika pirika za uchaguzi mkuu nchini Ujerumani ndizo mada zilizochambuliwa zaidi magazetini hii leo.

Kuhusu hali nchini Iran,gazeti la "Badische Zeitung linaandika:

Rais wa Marekani, Kansela wa Ujerumani na viongozi wengine wa magharibi wametamka hatimae kwamba uongozi wa Iran umevunja haki za binaadam na misingi ya demokrasia. Wametumia busara, kwasababu hawajaelemea upande wowote, badala yake wamekosoa mitindo iliyotumika. Hawataki kuupatia sababu utawala ya kuwasingizia wapinzani wake, wanashawishiwa kutoka nje. Lakini Ayatollah na mwanawe wa kulea hawahitaji sababu wao. Tangu mwanzo wamekua wakieneza propaganda dhidi ya nchi za Magharibi na Israel na sasa pia hali si nyengine. Hakuna uhakika hata kidogo kama sauti za kutoka magharibi zinaweza kuusaidia upande wa upinzani. Kuna haja ya sauti kupazwa kutoka nje hasa kwa kua hali hii inaoihusu jumuia nzima ya kimataifa."


Hayo ni maoni ya gazeti la Badische Zeitung la mjini Freiburg. Gazeti la Hamburger Morgenpost linaandika:

"Vitambaa vya kijani vinavyoashiria matumaini mema ya mageuzi ya amani nchini Iran vinazidi kugeuka vyekundu. Mzozo wa ugandanyifu wa uchaguzi uliosababishwa na Mahmoud Ahmedinedjad unamuathiri mwenyewe sasa kiongozi wa mapinduzi. Mamullah wengine wameshaanza kumgeukia Ayatollah Chamenei. Jee watamng'owa madarakani ili kuepusha uongozi wao wa kidini usitimuliwe kwa hasira za umma majiani?Hadi miezi ya hivi karibuni jambo hilo hakuna aliyekua akilifikiria, hivi sasa lakini kila kitu kinaweza kutokea."

Gazeti la Dresdner Neueste Nachrichten lina maoni mengine kabisa. Na linaaendelea kuandika:

"Matarajio, yawe mazuri vipi,kuona malalamiko ya umma mjini Teheran yakimalizikia kwa mageuzi ya mapinduzi ya amani, ni madogo mno. Hata kama watu wanaweza kulinganisha hali namna ilivyokua wakati wa utawala wa kiimla wa Erick Honnecker na huu wa Ayatollah Khamenei. Katika wakati ambapo mjini Leipzig serikali ilikua ikionyesha tuu maguvu yake bila ya kuyatumia, mjini Teheran utawala wa mamullah unayatumia kikatili dhidi ya vijana. Utawala unaojiendeleza kwa msaada wa nguvu za kijeshi,hauko mbali na kuporomoka. Kama si leo, kesho. Kwa namna hiyo, yaliyotokea Leipzig yanaweza pia kutokea Teheran.

Schäuble Kriminalstatistik 2008

Waziri wa mambo ya ndani Wolfgang Schäuble

Mada yetu ya pili inahusu wahka wa vyama vya kisiasa, katika wakati ambapo uchaguzi mkuu unakurubia humu nchini.Gazeti la SÜDKURIER la mjini Konstanz linaandika:

"Kishindo kilichosababishwa na matamshi ya Wolfgang Schäuble kuhusu uwezekano wa kuunda serikali ya muungano pamoja na walinzi wa mazingira, kinaonyesha kitu kimoja tuu: miezi mitatu kabla ya uchaguzi mkuu wahka unazidi kukua. Vyama ndugu vya CDU/CSU vinazidi kuingiwa na hofu pengine muungano pamoja na waliberali usijipatia kura za kutosha. Zaidi ya hayo, tangu uchaguzi wa bunge la Ulaya ulipomalizika,hofu zinazidi pia kuongezeka pengine FDP wakaendelea kuwavutia wapiga kura, tena wa kutoka upande wa CDU. Matamshi ya Wolfgang Schäuble hayakutolewa hivi hivi, yamelengwa kumzindua mwenyekiti wa Waliberali, Guido Westerwelle. Wakati huo huo matamshi hayo ni nasaha kwa vyama vyote vya kisiasa vikikumbushwa muungano unawezekana kati ya vyama vyote vya kidemokrasi.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/DPA

Mhariri:Othman Miraji

 • Tarehe 22.06.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/IWPX
 • Tarehe 22.06.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/IWPX