Maandamano nchini Zimbabwe. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 15.04.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Maandamano nchini Zimbabwe.

Wanajeshi na polisi wa Mugabe watanda nchini Zimbabwe kote ,wakati chama cha ipinzani MDC kinaandaa maandamano kupinga uamuzi wa mahakama kuu.

default

Katibu Mkuu wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe Tendai Biti

HARARE.

Majeshi yamewekwa  tayari  nchini Zimbabwe kote  wakati  maandamano yaliyoitishwa na chama cha upinzani yanatarijiwa kuanza kufanyika  leo nchini humo.

Chama  cha upinzani MDC kimeitisha maandamano  hayo kupinga uamuzi wa mahakama kuu ya Zimbabwe  kutupilia mbali rufaa ya chama hicho juu ya kuitaka  mahakama hiyo iiamrishe tume ya uchaguzi kutangaza   matokeo ya uchaguzi uliofanyika zaidi ya  wiki mbili zilizopita nchini  zimbabwe.

Jaji wa mahakama  kuu hiyo amesema matokeo ya  uchaguzi  hayatatangazwa mpaka  taarifa juu ya kosoro zilizojitokeza  katika kupiga kura zitakapochunguzwa.

Lakini makamu  mwenyekiti  wa chama cha MDC Thokozani Khupe  amesema maandamano yatafanyika

mpaka hapo matokeo ya uchaguzi yatakapotangazwa.


Wakati  huo  huo chama cha  upinzani MDC kimesema kuwa matendo ya kutumia nguvu yameenea nchini. Chama hicho kimefahamisha  kuwa msimamizi wake  mmoja  wa uchaguzi ameuliwa na wanamgambo wa   chama cha Mugabe ZANU- PF.


Na habari zaidi  zinasema kuwa Marekani na  Uingereza  zinakusudia kuliwasilisha suala la  Zimbabwe kwenye baraza la Usalama la Umoja wa  Mataifa hapo kesho licha ya upinzani  wa Afrika Kusini.


 • Tarehe 15.04.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Dhve
 • Tarehe 15.04.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Dhve
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com