1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano kumtetea karadzic

29 Julai 2008

Maandamano makubwa yamepangwa jioni ya leo mjini Belgrade,Serbia kuzuwia kupelekwa The Hague.

https://p.dw.com/p/ElqQ

Kiongozi wa waserbia nchini Bosnia,Radovan Karadzic anabidi kukabidhiwa Mahkama kuu ya Kimataifa juu ya uhalifu wa vita mjini The Hague, Holland,ili kukabili mashtaka.

Inatarajiwa mwishoni mwa wiki hii kufikishwa huko.

Wafuasi wa Karadzic,wanapanga leo jioni kuandamana kupinga kukabidhiwa kwake Mahkama hiyo.Maandamano hayo yameitishwa na chama chenye siasa kali cha kiserbia.

Swali linaloulizwa wakati huu ni je: wakili anaemtetea Radovan karadzic kweli amekabidhi hati ya kupinga kupelekwa mjini The Hague kwa mteja wake au kutangaza kwake kutuma barua dakika ya mwisho kwa njia ya posta ilikua sehemu ya njama zake za kuchelewesha kukabidhiwa Karadzic mahakama.

Hadi sasa mkakati huo umefanya kazi, kwani hukumu ya Mhakama maalumu ya Serbia juu ya hatima ya karadzic bado haikutolewa.

Kwahivyo, imebaki haifahamiki iwapo karadzic yupo bado mjini Belgrade, mji mkuu wa Jamhuri ya Serbia, ambako jioni ya leo maandamano makuu ya maalfu ya wakereketwa wa kiserbia yamepangwa kati kati ya mji huo.

Hatahivyo, taarifa za hivi punde zasema kwamba matayarisho yanafanywa na Mahkama ya mjini The Hague, kumpokea mshtakliwa.

1.Atmo/ O-Ton Rufe Radovan Karadzic

Swali hapa sio hatima ya Karadzic.Kwa chama cha Radical party cha Serbia,maandamano ya leo jioni ni fursa nzuri ya kutoa changamoto kwa rais Tadic wa Serbia, anaeelemea magharibi.

Miongoni mwa wafuasi wa chama hicho chenye siasa kali-Radical Party- ambaco kiliibuka na viti vingi katika uchaguzi uliopita lakini kiko upinzani,walitoa hata kitisho cha kumuua rais Tadic. Sasa hwachoki kusisitiza kwamba wanapanga maandamano ya amani jioni hii wakiwa na walinzi wao binafsi wa usalama.kuwashambuliwa wapiga-picha na wachukuaji filamu kama ilivyotokea wiki iliopita,haitatokea tena-alieleza Katibu mkuu wa chama Vucic.

""Tunawataka watu wote wanaopanga kushiriki katika maandamano haya, washiriki kwa amani. Waoneshe heshima kubwa na kutofautiana na wale watakao kuiteketeza Serbia.Hakuna mwenye ruhusa kulitia moto Bunge au kituo cha Tv cha serikali. Wala hakuna mwenye ruhusa kumnyonga muandishi habari,kwani afanyae hayo,anamsaidia tu Boris Tadic.Au ametumwa binafsi na Tadic."

Alidai katibu mkuu Vucic.

Jengo la bunge lililotiwa moto na kituo cha TV kilichowaka moto ilitokea hivyo wakati wa maandamano makubwa ya umma kutimua madarakani marehemu Slobodan Milosevic.Hiyo ndio maana anayokusudia Vucic.

Baadae akaja madarakani Voijslav Kostunica.

Lakini wakati umebadilika nchini Serbia.

Leo jioni Kuostunica wa chama cha Democratic Party

anawaungamkono wale wafuasi wanaoandamana kumtetea Karadzic.

Na wasoshalist wanaoongozwa na yule alieitwa "Slobo mdogo" Ivica Dacic,anatawala sasa pamoja na chama cha Boris Tadcic,hasimu wake wa zamani.