1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano kisiwani Madagascar

Oumilkher Hamidou29 Machi 2009

Wabuki wadai Ravalomanana arejee madarakani

https://p.dw.com/p/HM8i

Antananarivo:


Rais aliyetimuliwa madarakani kisiwani Madagascar,Marc Ravalomanana amewaahidi kwa mara nyengine tena wafuasi wake"wataonana haraka".Ravalomanana amesema hayo katika risala iliyochapishwa leo na vyombo vyake vya habari."Msiwe na hofu,nitarejea haraka ,kufanya kazi kwaajili ya ufanisi" amesema hayo rais huyo aliyelazimika kujiuzulu March 17 iliyopita.Tangu jumatatu iliyopita,wafuasi wake wamekua wakiandamana mjini Antananarivo kulaani kuingia madarakani kiongozi wa zamani wa upinzani,Andry Rajoelina wakitoa mwito katiba iheshimiwe.Katika maandamano ya jana polisi wamepambana na maelfu ya wafuasi wa Ravalomanana.Watu wasiopungua 30 wamejeruhiwa pale polisi walipojaribu kuwazuwia waandamanaji katika mji mkuu Antananarivo.Kiongozi mpya wa Madagascar,Andry Rajoelina amewaambia maripota atazingatia ratiba ya kuitisha uchaguzi.Nchi nyingi za dunia zimelinganisha kisa cha kuingia madarakani Rajaoelina na njama ya mapinduzi na kutoa mwito uchaguzi utishwe haraka iwezekanavyo.