Maambukizi ya homa ya nguruwe yabadilika | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 30.04.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Maambukizi ya homa ya nguruwe yabadilika

Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limeongeza makali ya tahadhari ya ugonjwa wa homa ya nguruwe hadi awamu ya tano japokuwa bado halijakuwa janga la kimataifa

default

Keiji Fukuda,Mratibu wa mpango wa kupambana na Influenza WHO


Onyo hilo lina maana kuwa ugonjwa huo unaweza kusambazwa kati ya binadamu vilevile kati ya mataifa mawili kwa uchache.Hilo limesisitizwa na Mkuu wa Usalama wa Afya wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO Keiji Fukuda aliyesema kuwa ''Kwa sasa hakuna ushahidi wowote unaonyesha kuwa virusi hivi vinasambaa kutoka kwa nguruwe hadi binadamu.Virusi hivi vinaonekana kuwa vinasambaa kutoka mtu mmoja hadi mwengine.''Schweinegrippe Mexico

Wakazi wa Mexico wapimwa viwango vya joto mwilini

Kwa sasa mataifa hayo mawili ni Marekani na Mexico ambako ndiko chanzo cha virusi hivyo.

Kwa mujibu wa taarifa mtu mmoja amethibitishwa kuwa amefariki kwasababu ya homa hiyo nchini Marekani na wengine 91 wameambukizwa.Vifo 159 vya kwanza vimeripotiwa kutokea nchini Mexico na watu wengine 2500 tayari wameambukizwa virusi hivyo nchini humo.Kwa sasa watu wengine kadhaa wameripotiwa kuambukizwa virusi vya homa ya nguruwe katika mataifa mengine 26 kote ulimwenguni.


Katika bara la Ulaya visa vipya vya maambukizi vimeripotiwa na kuthibitishwa katika nchi za Ujerumani na Austria.Mpaka sasa watu watatu wameambukizwa virusi hivyo hapa Ujerumani,mmoja huko Austria,watano Uingereza na wengine 10 Uhispania.Mataifa mengine barani Ulaya yako chonjo na yanachukua tahadhari zinazohitajika.

Mwandishi:Thelma Mwadzaya /RTRE

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com