1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafisa wawili wa polisi wauwawa

11 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D5sp

Maafisa wawili wa polisi wameuwawa katika shambulio la bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara kaskazini mwa Sri Lanka hii leo.

Shambulio hilo huenda limefanywa na waasi wa Tamil Tigers.

Duru za jeshi la nchi hiyo zinasema idadi ya vifo vilivyosababishwa na mapigano ya mwishoni mwa juma imeongezeka na kufikia waasi 75 na wanajeshi saba.

Mapigano kati ya jeshi la Sri Lanka na waasi wa Tamil Tigers yameongezeka tangu serikali ilipofutilia mbali mwezi uliopita mkataba wa kusitisha mapigano uliokuwa umedumu kwa muda wa miaka sita.

Serikali inasema waasi wa Tamil Tigers walikuwa wakiutumia muda wa usitishwaji mapigano kujihami.