Müller, Lahm wasaini mikataba mipya na Bayern | Michezo | DW | 11.06.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Müller, Lahm wasaini mikataba mipya na Bayern

Thomas Müller na Philipp Lahm wamesaini mikataba mipya itakayowaweka katikam klabu ya Bayern Munich hadi mwaka wa 2019 na 2018. Wachezaji hao wako Brazil katika kikosi cha Ujerumani cha Kombe la Dunia.

Mkataba wa nahodha Lahm sasa utakamilika mwaka wa 2018 wakati naye Müller akisalia katika klabu hiyo kwa miaka mitano ijayo. Wachezaji hao wawili waliimarika na kupandishwa ngazi kutoka shule ya mafunzo ya Bayern wakati Lahm akiwa na miamba hao wa Bavaria tangu miaka 11 iliyopita.

Afisa mkuu mtendaji wa Bayern Karl-Heinz Rummenige amesema Lahm na Mäller ni sehemu muhimu ya Bayern Munich. Wamesalia kuwa waaminifu kwa klabu hiyo tangu mwanzoni mwa kazi yao ya soka na pia wataendelea kutekeleza jukumu kubwa katika klabu hiyo bingwa wa Ujerumani.

Kuthibitishwa mikataba ya wachezaji hao wawili kumemaliza uvumi uliodumu wiki kadhaa kuhusiana na hatima ya mshambuliaji Müller mwenye umri wa miaka 24 ambaye alikuwa akidaiwa kuihama klabu hiyo.

Müller amekuwa na klabu ya Bayern kwa miaka 14 iliyopita na amesema uhusiano alio na miamba hao ndio sababu iliyomfanya kusaini mkataba mpya.

Wachezaji hao wawili wako katika kikosi cha Ujerumani chake Kocha Joachim Löw kinacholenga kupambana na timu nyingine katika Kombe la Dunia nchini Brazil na matarajio ya kuleta nyumbani Kombe lao la nne la dunia.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Josephat Charo