LUXEMBOURG: Rais Mugabe hatoalikwa mkutano wa Novemba | Habari za Ulimwengu | DW | 19.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LUXEMBOURG: Rais Mugabe hatoalikwa mkutano wa Novemba

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ureno,Luis Amado amesema,Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe hatoalikwa kwenye mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika,unaotarajiwa kufanywa mwezi Novemba katika mji mkuu wa Ureno, Lisbon. Waziri huyo,amenukuliwa akisema kwamba hana hamu ya kumuona Mugabe mjini Lisbon kwa sababu atakuwa chanzo cha matatizo.Rais Mugabe na zaidi ya maafisa 100 wa Zimbabwe walio karibu na utawala wake,wamewekewa vikwazo vya usafiri katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya.Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya Mugabe kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa rais mwaka 2002.Watazamaji wa kimataifa walisema,uchaguzi huo ulikuwa wa udanganyifu na visa vya kuandama na kukandamiza wapinzani.Baadhi ya viongozi mashuhuri barani Afrika,wamepinga hatua yo yote ya kumzuia Rais Mugabe kuhudhuria mkutano huo wa kilele kati ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com