1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Luxembourg. Mazungumzo ya kuingiza Uturuki katika EU yaahirishwa.

3 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEVO

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya wameahirisha kikao chao cha mazungumzo ya dharura mjini Luxembourg kwa usiku wa leo.

Mkutano huo wenye lengo la kumaliza mkwamo juu ya mazungumzo ya kuiingiza Uturuki katika umoja wa Ulaya yataendelea leo Jumatatu.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Jack Straw ameyaita mazungumzo hayo ya uanachama wa umoja wa Ulaya kwa Uturuki kuwa ni muhimu , akisema kuwa kile kinachopendekezwa kwa Uturuki kuwa ni hali ya kushindwa kwa umoja huo.

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesisitiza kuwa viongozi wa umoja huo ni lazima waamue iwapo umoja wa Ulaya ujipatie nafasi ya kuwa nguvu kuu katika dunia ama ibaki kuwa klabu ya Wakristo.

Uturuki imetishia kususia mazungumzo ya leo Jumatatu iwapo umoja huo utakubali wito wa Austria wa kuipatia Uturuki nafasi ya kuwa mshirika mpendelewa, badala ya kuwa mwanachama kamili wa umoja huo.