LUSAKA:Waziri wa ardhi afukuzwa kazi | Habari za Ulimwengu | DW | 01.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LUSAKA:Waziri wa ardhi afukuzwa kazi

Rais wa Zambia Levy Mwanawasa amemfukuza kazi waziri wa Ardhi kufuatia madai ya maafisa wa ngazi za juu katika wizara yake kuhusika na vitendo vya rushwa.Hakuna sababu yoyote iliyotolewa kufuatia hatua hiyo ya kufukuzwa kazi kwa Gladys Nyirongo.Taarifa zinaeleza kuwa maafisa wa ngazi za juu wamekuwa wakitoa ardhi kinyume na sheria na kupokea hongo.

Kulingana na msemaji wa Rais Mwanawasa, John Musukuma,naibu waziri wa sheria Bradford Machila ameteuliwa kuchukuwa nafasi hiyo.

Rais Mwanawasa kwa upande wake anaripotiwa kutangaza kuwa wizara ya ardhi inakabiliwa na vitendo vya rushwa na aliahidi kurekebisha hali hiyo.Kiongozi huyo aliahidi kupambana na rushwa nchini mwake na kuonya kumfuta kazi yeyote atakayepatikana na hatia.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com