1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA: Rais Mwanawasa atoa mwito kuwe na utulivu

2 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6x

Rais wa Zambia, Levy Mwanawasa, amewatolea mwito raia wawe na utulivu huku matokeo ya mwisho rasmi ya uchaguzi yakitarajiwa kutangazwa baadaye leo.

Machafuko yalizuka mjini Lusaka baada ya maofisa wa uchaguzi kuchelewa kutangaza matokeo. Wafuasi wa upinzani waliokuwa na hasira walizifunga barabara mjini humo kwa kuchoma matairi na kuwashambulia maofisa wa polisi kwa mawe.

Kufuatia kuhesabiwa kwa kura hapo jana, rais Mwanawasa alimshinda mpinzani wake mkuu Michael Sata, ambaye amekuwa akiongoza katika matokeo ya awali. Sata sasa anashikilia nafasi ya tatu, nyuma ya kiongozi wa muungano wa United Democratic, Hakainde Hichilema.

Upinzani unasema kumekuwa na mizengwe lakini rais Mwanawasa alisema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki wakati alipolihutubia taifa hapo jana.