LUSAKA: Mwanawasa atangazwa mshindi wa uchaguzi | Habari za Ulimwengu | DW | 03.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LUSAKA: Mwanawasa atangazwa mshindi wa uchaguzi

Tume ya uchaguzi nchini Zambia imemtangaza rais Levy Mwanawasa kuwa mshindi wa uchaguzi nchini humo. Rais Mwanawasa ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 43 ya kura. Aidha tume ya uchaguzi imesema mpinzani wa rais Mwanawasa, Michael Sata, amepata asilimia 30 ya kura.

Sata amewatolea mwito wafuasi wake wawe watulivu kufuatia siku mbili za maandamano katika maeneo ya mitaa ya walalahoi mjini Lusaka.

Sata amemlaumu rais Mwanawasa kwa kuiba ushindi lakini akasema atakubali ameshindwa na wala hatawasilisha mashtaka katika mahakama kuu ya kutaka uchaguzi mwingine ufanywe.

Nafasi ya tatu ilichukuliwa na Hakainde Hichilema aliyepata asilimia 25 ya kura.

Hapo jana benki na biashara zilifungwa wakati polisi walipokuwa wakikabiliana na waandamanaji waliokuwa wakifanya fujo mjini Lusaka.

Machafuko yaliripotiwa pia mjini Kitwe katika eneo lenye migodi ya shaba.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com