1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA: Mpango wa dharura kwa wakimbizi wa Zimbabwe

19 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXh

Shirika la Umoja wa Mataifa-UNHCR linalohudumia wakimbizi duniani,limeandaa mpango wa dharura, ikitarajiwa kuwa maelfu ya Wazimbabwe watakimbia hali ya kisiasa na kiuchumi inayozidi kuwa mbaya nchini mwao.

Mkuu wa UNHCR,Antonio Guterres akiwa nchini Zambia kutathmini hali ya wakimbizi amesema, Wazimbabwe wanaoikimbia nchi hiyo wanahitaji misaada ya kiutu,hata ikiwa hawakuomba hifadhi. Akaongezea kuwa hadi hivi sasa,zaidi ya Wazimbabwe milioni 3 wameihama nchi yao,lakini ni wachache tu walioomba hifadhi katika nchi za jirani.Kwa mujibu wa takwimu rasmi za uhamiaji,kiasi ya Wazimbabwe 1,000 wameingia Zambia.