1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Luka Modric kukimbilia Inter ?

Sekione Kitojo
2 Agosti 2018

Baada  ya  Cristiano Ronaldo  kuondoka Real Madrid  kwenda Juventus , nyota  wa  Croatia Luka  Modric huenda  akawa mchezaji mwingine  kuamua  kuondoka  katika  mji  mkuu  wa  Uhispania kwenda  katika  ligi  ya  Serie A.

https://p.dw.com/p/32XPm
Russland WM 2018 Frankreich gegen Kroatien
Luka Modric nahodha wa CroatiaPicha: Reuters/K. Pfaffenbach

Siku  ya  Alhamis  gazeti  la  michezo  la  Italia  Gazzetta dello Sport limeripoti kwamba  Vanja Bosnic, mke wa  Modric  na  meneja  wake, ameiuliza  Inter Milan  iwapo  ina  haja  na  mchezaji  huyo. "Raia huyo  wa  Croatia  anataka  kwenda  katika  kikosi  hicho  cha Nerazzurri  lakini  hali ni  ya  mkanganyiko,"  gazeti  hilo  limesema.

Mchezaji  huyo  wa  kati  Modric  mwenye  umri  wa  miaka  32 lakini gharama  zake  za  uhamisho zitaleta  matatizo  kwa  Inter baada  ya kufanya  vizuri  sana  katika  kombe  la  dunia  na  jukumu  lake muhimu  katika  kushinda  vikombe  kadhaa  vya  Champions League kwa  Real Madrid.

Modric ana  makataba  na  Madrid  hadi  mwaka  2020  lakini  Inter itamuunganisha  na  mchezaji  mwenzake  kutoka  Croatia  Ivan Perisic , Marcelo Brozovic na  mchezaji  mpya  Sime Vrsaljko.