Lotus kutumia injini za Mercedes msimu ujao | Michezo | DW | 10.10.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Lotus kutumia injini za Mercedes msimu ujao

Katika mashindano ya magari ya Formula One, Timu ya Lotus imetangaza kuwa itaacha kutumia injini za Renault kwenye magari yake na badala yake itatumia injini za kampuni ya Mercedes 2015.

Timu hiyo inamaliza uhusiano wa muda mrefu na kampuni ya Renault na kuingia katika kampuni inayotengeneza injini zenye ufanisi mkubwa katika mbio za magari ya Formula 1 ili kujaribu kuimarisha ushindani wake.

Timu ya Lotus ilimaliza katika nafasi ya nne katika kitengo cha ujenzi wa injini bora yaani constructors katika msimu uliopita lakini imeshuka hadi nafasi ya nane mwaka huu.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu