1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lorenco tena Angola

29 Agosti 2022

Tume ya uchaguzi nchini Angola imemtangaza rais Joao Lorenco wa chama tawala cha MPLA kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofaanyika wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/4GBlz
Angola Luanda Wahlkampfveranstaltung der MPLA | Präsident Joao Lourenco
Picha: JULIO PACHECO NTELA/AFP

Matokeo hayo yanakirejesha mamlakani chama hicho kilichoongoza kwa miaongo mitano nchini humo. soma Waangola kuamua kati ya Lourenco na Costa Junior

 

Kulingana na tume hiyo ya uchaguzi, chama cha MPLA kimeshinda kwa wingi wa asilimia 51.17 baada ya kura zote kuhesabiwa, huku mpinzani wa chama hicho UNITA kikiibuka na ushindi wa asilimia 43.95, haya yakiwa ni matokeo ya ju ú kabisa kwa chama hicho kuwahi kuyapata.

Hata hivyo ni watu wachache waliripotiwa kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi huo wa Jumatan iliyopita, ambao licha ya wagombea kuchuana vikali, lakini bado umekirejesha madarakani chama tawala cha MPLA kilichotawala kwa zaidi ya miaka 50, tangu taifa hilo lilipopata uhuru wake kutoka kwa Ureno mwaka 1975.

soma Angola: MPLA yatangazwa mshindi, UNITA yakataa matokeo

UNITA walipinga matokeo ya awali

 UNITA leader speaks to journalists
Vuiongozi wa UNITA katika mkutano na waandishi wa habariPicha: António Cascais/DW

Kiongozi wa UNITA Adalberto Costa Juniour ameyakataa matokeo hayo, akiangazia tofauti iliyojitokeza kwenye hesabu ya kura kati yao na tume ya uchaguzi. hata hivyo hakupatikana kueleza chochote kuhusiana na tangazo hilo la mwisho la matokeo ya uchaguzi.

Wachambuzi wanahofia kwamba hatua yoyote ya kukataa matokeo inaweza kuchochea maandamano makubwa ya watu na hususan wa tabaka la chini na vijana ambao kwa kiasi kikubwa walimpigia kura Juniour.

soma Raia wa Angola wapiga kura katika kinyang'anyiro kikali

Ushindi wa chama cha MPLA 

Angola Cabinda | Bekanntgabe der Wahlergebnisse
AngolaPicha: Simão Lelo/DW

Tangazo la tume ya uchaguzi linatolewa siku moja baada ya mazishi ya aliyekuwa rais wa muda mrefu wa taifa hilo Jose Eduardo dos Santoswa chama cha MPLA aliyefariki dunia nchini Uhispania mwezi Julai. Usalama kwenye mji mkuu Luanda ungali umeimarishwa.

Usiku wa Jumamosi wajumbe watano kati ya 16 wa tume hiyo ya uchaguzi walitishia kutosaini matokeo ya awali ambayo yaliyoonyesha chama hicho cha MPLA kikiongoza kwa asilimia 51.07 ya kura zote, huku Chama kikuu cha upinzani cha UNITA kikiwa na asilimia 44.05.

Alipozungumza pembezoni mwa shughuli ya mazishi ya aliyekuwa rais wa muda mrefu wa taifa hilo Jose Eduardo dos Santos mjini Luanda, kiongozi wa UNITA Adaberto Costa Juniour alisema angeyakubali matokeo iwapo yatafanana na hesabu ya kura iliyofanywa na chama chake. Alisema tayari walikuwa wamewasilisha malalamiko kwenye tume ya uchaguzi.

Matokeo haya ya sasa yanamrejesha kwa awamu ya pili rais Joao Lorenco aliyepokea kijiti kutoka kwa hayati Eduardo Dos Santos mwaka 2017.

 

AFPE/RTRE