LONDON:Wajumbe wa nchi tano za baraza la usalama washindwa kufikia uamuzi juu ya Iran | Habari za Ulimwengu | DW | 27.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON:Wajumbe wa nchi tano za baraza la usalama washindwa kufikia uamuzi juu ya Iran

Wajumbe wa nchi tano wanachama wa kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa pamoja na Ujerumani waliofanya mazungumzo hapo jana nchini Uingereza walishindwa kufikia uamuzi kuhusu hatua za kuchukuliwa juu ya Iran baada ya nchi hiyo kukataa kukomesha mpango wake wa Kinuklia.

Wajumbe hao wanatajariwa kuendelea na mazungumzo yao juu ya suala hilo baadae wiki hii.

Mkutano wa hapo jana ulikuja baada ya shirika la kimataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya Atomiki kuthibitisha kwamba Iran imepuuza muda wa mwisho uliowekwa kusimamisha shughuli zake za kinyuklia.

Muda huo ulimaliza wiki iliyopita.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com