LONDON:Uingereza yasema saa 48 zitatoa majaaliwa ya mzozo wa wanamaji wake wanaoshikiliwa Iran | Habari za Ulimwengu | DW | 03.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON:Uingereza yasema saa 48 zitatoa majaaliwa ya mzozo wa wanamaji wake wanaoshikiliwa Iran

Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema kuwa saa 48 zijazo zitakuwa ngumu katika kutafuta suluhisho la kadhia ya kukamatwa na Iran wanamaji wake 15.

Tony Blair amesema kuwa mazungumzo kati ya nchi hizo yanatoa mwanga wa kupatikana kwa suluhisho, lakini hata hivyo akasema la muhimu ni kwa wanamaji hao kuachiwa.

Mapema Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Iran, Ali Larajani akizungumza na televisheni ya Uingereza amesema kuwa wanamaji hao huenda wakaachiwa huru bila ya kushtakiwa.

Wakati huo huo mwanadiplomasia wa kiiran aliyekuwa ametekwa huko Baghdad ameachiwa huru na amewasili mjini Tehran.

Afisa huyu wa kibalozi wa Iran Jala Sharafi alitekwa na watu waliyokuwa wamevalia sare za jeshi la Iraq tarehe 4 mwezi January mwaka huu.

Hayo yakiendelea mkutano uliyokuwa ufanyike leo kati ya waandishi wa habari na rais Mahamoud Ahmed nejad umeahirishwa hadi kesho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com