1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Tonny Blair kung´atuka rasmi uwaziri Mkuu

27 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBnq

Waziri Mkuu wa Uingereza Tonny Blair muda mfupi ujayo anastaafu kutoka katika nafasi hiyo na kumpisha waziri wa fedha Gordon Brown kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza.

Muda mfupi baadaye Tonny Blair anatarajiwa kutangazwa kuwa mjumbe maalum katika mzozo wa mashariki ya kati.

Pande nne zinazoshughulika na kusaka amani katika mashariki ya kati, zilimaliza mazungumzo yao mjini Jerusalem bila ya kumtangaza mjumbe mpya atakayesimamia utafutaji wa amani katika eneo hilo.Tonny Blair alikataa kuzungumzia juu ya uvumi huo wa yeye kuchukua nafasi hiyo.

Hata hivyo mwakilishi wa Umoja wa Ulaya katika mazungumzo hayo, alisema kuwa Blair amepewa nafasi kubwa na wajumbe wa mkutano huo, na kwamba uamuzi utatangazwa leo.

Pande hizo nne za kutafuta amani mashariki ya kati zinaundwa na Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa, Urusi na Marekani.