LONDON:Shirika la Kutetea haki za binadamu lataka NATO iache kupeleka wafungwa Afghanistan | Habari za Ulimwengu | DW | 13.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON:Shirika la Kutetea haki za binadamu lataka NATO iache kupeleka wafungwa Afghanistan

Shirika la kutetea haki za binadamu duniani Amnesty International limetoa mwito kwa nchi za NATO zinazolinda amani nchini Afghanistan kuacha kupeleka wafungwa nchini humo.

Shirika hilo limesema katika ripoti yake kwamba wafungwa hao wanateswa wanapoingia katika mikono ya maafisa wa Afghanistan

Asasi hiyo ya kupigania haki za binadamu pia imesema , nchi za NATO zinafumbuia macho mateso kwa kuendelea kupeleka wafungwa katika jela za Afghanistan.

Amnesty International imekariri inachoita matendo ya mateso na kukiukwa haki za binadamu yanayofanywa na idara za usalama za Afghanistan.

Sheria ya kimataifa inapiga marufuku kupeleka wafungwa katika sehemu ama nchi ambapo mateso ama ukiukaji wa haki za binadamu wa aina yoyote unatuhumiwa kutendeka.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com